
Marekani itaweka vizuizi nchini Venezuela dhidi ya “meli za mafuta zilizowekewa vikwazo zinazoingia na kutoka Venezuela,” Rais Donald Trump ametangaza. Hii inaashiria ongezeko jipya la mgogoro kati ya nchi hizo mbili.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mvutano kati ya Marekani na Venezuela umeongezeka. Siku ya Jumanne, Desemba 16, Donald Trump ametangaza kwenye mtandao wake wa Truth Social kwamba Marekani imrkuwa ikiweka vizuizi nchini Venezuela dhidi ya “meli za mafuta zilizowekewa vikwazo.”
“Leo, ninaamuru vizuizi kamili vya meli zote za mafuta zilizowekewa vikwazo zinazoingia na kutoka Venezuela,” rais wa Marekani ameandika, kwani mafuta ndiyo chanzo kikuu cha mapato cha Caracas.
“Rais wa Marekani anajaribu, kwa njia isiyo na mantiki kabisa, kuweka kile kinachoitwa kizuizi cha kijeshi cha majini dhidi ya Venezuela ili kuiba utajiri ambao ni wa nchi yetu,” serikali ya Venezuela imejibu katika taarifa.
Kwa kuzingatia vikwazo tangu mwaka 2019, nchi inauza uzalishaji wake wa mafuta kwenye lisilo rasmi kwa bei ya chini sana, hasa kwa China.
Utawala wa Rais Nicolas Maduro unatumia mafuta kufadhili “ugaidi wa dawa za kulevya, biashara haramu ya binadamu, mauaji, na utekaji nyara,” Donald Trump amedai.
Venezuela “imezungukwa na silaha kubwa zaidi katika historia ya Amerika Kusini”
Utawala wa Marekani unamtuhumu Nicolas Maduro kwa kuongoza mtandao mkubwa wa biashara haramu ya dawa za kulevya, jambo ambalo analikanusha vikali, akidai kwamba Washington inajaribu kumpindua ili kunyakua mafuta ya nchi yake.
Marekani imepeleka kikosi kikubwa cha kijeshi katika Karibiani na kushambulia meli zinazoshukiwa kuwa na biashara haramu ya dawa za kulevya kutoka Venezuela.
“Venezuela imezungukwa kabisa na silaha kubwa zaidi kuwahi kukusanywa katika historia ya Amerika Kusini,” bilionea huyo wa Republican ametangaza, akiongeza kuwa idadi ya wanajeshi a Marekani wanaotumwa huko “itaongezeka tu.”
“Pigo watakalolipata litakuwa la kipekee,” ametishia.