
Tangazo la kundi la waasi wa AFC/M23, mashariki wa DRC, ambalo liliwekwa hadharani usiku wa Jumatatu, Desemba 15 kuamkia Jumanne, Desemba 16, ambalo utekelezaji wake unategemea masharti kadhaa—linaacha maswali mengi bila majibu. Miongoni mwao ni: muda gani wa kujiondoa? Wigo wake utakuwaje? Na ni “kikosi gani kischoegemea upande wowote” kitakacho “fuatilia usitishaji mapigano”?
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tangazo lililotolewa na AFC/M23 saa 7:30 usiku wa Jumatatu, Desemba 15 kuamkia Jumanne, Desemba 16, la kujiondoa kwa masharti kutoka Uvira, mji wa pili kwa ukubwa katika mkoa wa Kivu Kusini mashariki mwa DRC, halijabainika wazi kama lilivyoweza kuonekana mwanzoni. Ingawa kundi hili linadai kutaka “kutoa nafasi nzuri kwa mchakato wa amani” wa Doha na linasema linajibu ombi kutoka kwa mpatanishi, Marekani, maswali kadhaa yanabaki kuhusu utekelezaji wa uamuzi wake.
La kwanza linahusu muda sahihi wa kujiondoa huku: kundi hili la waasi halikutangaza tarehe yoyote ya kujiondoa kwake katika mji wa Uvira, na ni muhimu kuzingatia kwamba, wapiganaji wake bado walikuwepo katika mitaa ya Uvira siku ya Jumanne usiku. Zaidi ya hayo, halitoi dalili yoyote ya wazi ya umbali wa kurudi nyuma kwake: AFC/M23 inataja hilo kwa ajili ya mji wa Uvira, lakini si kwa ajili ya eneo la Uvira, eneo kubwa la kiutawala. Ikiwa itajiwekea kikomo cha kujiondoa katika mji wa Uvira pekee, kwa hivyo itahifadhi sehemu kubwa ya utawala katika maeneo iliyoteka katika siku za hivi karibuni: Luvungi, ambayo kwa muda mrefu imekuwa sehemu ya kimkakati kwa FARDC katika eneo hilo, na pia Sange, kaskazini, na Makobola na Mboko, kusini.
Mamlaka za juu zaidi za Marekani imearifiwa kuhusu hali hiyo
“M23 itaondoka Uvira, lakini mpaka wapi? Mpaka Kamanyola? Mpaka Bukavu? Hatujui kwa usahihi. Zaidi ya hayo, uamuzi huu una masharti ya kuondoa jeshi katika eneo hilo: je, hii ina maana kwamba taifa la Kongo litarejesha udhibiti bila kuanzisha mamlaka yake? Hilo haliwezekani: serikali ya Kongo bila shaka itataka kupeleka jeshi lake na vikosi vya usalama ili kuwalinda raia. Kwa hakika tunaweza kutetea kuanzishwa kwa kikosi kisichoegemea upande wowote, lakini ni nani asiyeegemea upande wowote katika muktadha wa sasa?” anahoji Josué Kayeye, mwanachama wa shirika la kiraia katika mkoa wa Kivu Kusini.
Masharti yaliyowekwa na M23 yanatia shaka utekelezaji halisi wa kujiondoa kwake.
Kulingana na masharti kadhaa ambayo kundi hilo linazingatia dhamana ya usalama, kujiondoa kwa AFC/M23 kutoka Uvira sasa kutategemea jinsi wadhamini wa makubaliano ya amani yaliyosainiwa kati ya DRC na Rwanda huko Washington watakavyoshirikiana katika kuendeleza mbinu zake halisi na wadau. Alipoulizwa kuhusu suala hilo mjini Kinshasa, Balozi wa Marekani, Lucy Tamlyn, alibaini kwamba mamlaka za juu zaidi za Marekani ziliarifiwa kuhusu hali hiyo. “Tutaendelea kufanya mazungumzo na pande zote na kusisitiza umuhimu wa kurudi kwenye mfumo wa mazungumzo uliowekwa,” alisema.
Makubaliano haya yanatoa mifumo miwili: kwanza, Mfumo wa Pamoja wa Uratibu wa Usalama (JSCM) wenye lengo la kiutendaji kati ya DRC na Rwanda; Kwa upande mwingine, kuna Kamati ya Pamoja ya Ufuatiliaji ambayo inapokea usaidizi kutoka Marekani, Qatar na Umoja wa Afrika na ambayo dhamira yake ni kufuatilia utekelezaji wa makubaliano kwa ujumla, kuchunguza malalamiko na kutatua mizozo.