Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. Said Mtanda, amewahimiza viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kuendelea kujadili changamoto za elimu kwa uwazi na uwajibikaji, ili kuleta maendeleo katika sekta ya elimu na taifa.

Ujumbe wa RC Mtanda umetolewa Kwenye Mkutano mkuu wa watumishi wa CWT kutoka pande zote za Nchi ambao unafanyika kwa siku mbili jijini Mwanza

Mkutano huu utatumika kuwachagua viongozi wa tawi la watumishi wa CWT watakaoongoza kwa mwaka 2025 hadi 2030. NA RC Mtanda akawakumbusha kuhakikisha wanazifikisha kwa uwazi changamoto zote za walimu na tasnia ya elimu kwa mamlaka husika bila kuchoka.

Risala ya Watumishi wa CWT kupitia katibu Mkuu wao Joseph Misalaba iliyowasilishwa mbele ya Serikali ya Mkoa wameahidi kuendelea kuisimamia taaluma ya ualimu kwa weledi huku wakiamini serikali itaendelea kuboresha maslahi yao.

Walimu hao pia wametambua jitihada mamlaka kuendelea kuatatua changamoto za elimu na Shukrani zao zimetolewa na Mwalimu Suzan Shesha – Katibu CWT- Pwani pamoja na Mwalimu Heri Mtovano – Katibu CWT -Mbozi-Songwe

Mkutano huu unasimamiwa na kaulimbiu ya nguvu moja sauti moja na maumivu ya mmoja ni maumivu ya wote.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *