#HABARI:Serikali ya Kaunti ya Nairobi nchini Kenya imeidhinisha rasmi utaratibu wa kutoa siku mbili kila mwezi za kupumzika kwa sababu ya hedhi kwa wanawake wafanyakazi, kama sehemu ya mfumo wa rasilimali watu wa kaunti hiyo.

Uamuzi huu umefikiwa baada ya kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Gavana wa jimbo hilo Johnson Sakaja, kilichopendekeza kuingiza usaidizi wa afya ya hedhi katika sera za rasilimali watu, kwa lengo la kuboresha ustawi wa wafanyakazi na kuongeza utendakazi wawanawake kazini.

Taarifa ya kaunti inabainisha kuwa changamoto za afya ya hedhi, hususan dysmenorrhea (maumivu makali ya hedhi), huathiri kwa kiasi kikubwa ustawi wa wanawake na utendaji wao kazini.

Tafiti zinaonyesha kuwa kati ya wanawake 65 hadi 80 kwa mia hukabiliwa na maumivu ya hedhi, na idadi kubwa ufanisi wao kazini huathirika zaidi.

Kwa kuwa wanawake wanajumlisha zaidi ya nusu ya wafanyakazi wa Kaunti ya Nairobi, changamoto hizi zinachangia kupungua kwa ufanisi, kuwepo kazini licha ya ugumu wa kiafya (presenteeism) na kuathiri huduma za umma.

Sera mpya itawaruhusu wanawake kusitisha kazi kwa siku mbili kila mwezi bila kuongeza mzigo wa kifedha kwa kaunti, na hivyo kutoa msaada wa kimuundo kwa wafanyakazi.

Nchi nyingine zilizo na haki za likizo ya hedhi ni pamoja na Zambia, Japan na Korea Kusini-ambapo Sheria ya Viwango vya Kazi inawataka waajiri kutoa siku moja ya likizo ya hedhi kwa mwezi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *