k

Chanzo cha picha, Reuters

    • Author, Will Grant
    • Nafasi, BBC

Mvutano unaoongezeka kati ya Marekani na Venezuela umesababisha ongezeko kubwa zaidi la wanajeshi katika eneo la Caribbea tangu kumalizika kwa Vita Baridi.

Mara ya mwisho meli nyingi za kivita za Marekani na wanajeshi kutumwa katika eneo hilo ilikuwa mwaka 1989, wakati Washington ilipomwondoa madarakani Rais wa Panama, Manuel Noriega – ambaye ilimshutumu kwa biashara haramu ya dawa za kulevya.

Tarehe 16 Desemba 1989, Luteni wa Jeshi la Wanamaji la Marekani Robert Paz alikuwa Chevrolet Impala akielekea Hoteli ya Marriott huko Panama City kwa chakula cha jioni, huku mvutano wa Marekani na rais wa Panama ukifikia kiwango kikubwa.

Gari hilo, ambalo lilikuwa limebeba wanajeshi wanne wa Marekani waliokuwa nchini humo, lilipofika kwenye kituo cha ukaguzi cha Jeshi la Ulinzi la Panama, wanajeshi sita walilizunguka gari hilo.

Kufuatia ugomvi, Wapanama walifyatua risasi walipokuwa wakiondoka, na kumuua Paz. Kifo chake kilisababisha uvamizi wa Marekani dhidi ya Panama siku nne baadaye, tarehe 20 Desemba.

Inasalia kuwa uvamizi mkubwa na wa mwisho wa Marekani katika ardhi ya kigeni huko Amerika.

Kufikia mwisho wa kile ambacho Washington ilikiita “Operesheni Just Cause,” takriban wanajeshi 30,000 wa Marekani walikuwa huko, na Noriega alilazimishwa kutoka madarakani na kupelekwa Miami kukabiliana na mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya.

Umoja wa Mataifa unakadiria takriban raia 500 wa Panama waliuawa katika uvamizi huo. Marekani inadai idadi ilikuwa ndogo zaidi, wakisema idadi hiyo ni kubwa sana.

Kulikuwa na ita vya maneno kati ya Washington na kiongozi huyo wa Amerika Kusini na ndivyo vilivyosababisha kupelekwa kwa wanajeshi wa Marekani katika eneo hilo.

Venezuela na Panama zote zinatuhumiwa na Washington kwamba marais wao wanahusika katika biashara haramu ya dawa za kulevya.

Mataifa yote mawili pia yana umuhimu mkubwa wa kimkakati – katika Mfereji wa Panama na akiba kubwa ya mafuta ya Venezuela.

Pia unaweza kusoma

Tofauti ya Panama na Venezuela

l

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati ule ulikuwa ni wa Vita Baridi na sasa ni Karne ya 21, George HW Bush – alikuwa kiongozi nchini Marekani mwaka 1989 – na Donald Trump ni kiongozi wa sasa.

Noriega alikuwa akitumiwa na CIA kwa miaka mingi na hatimaye alihukumiwa kwa ushahidi usiopingika ambao ulianzia kwenye rekodi za kifedha hadi ushuhuda kutoka kwa wanaume waliokuwa wakiendesha ndege za dawa za kulevya au kutakatisha pesa za dawa za kulevya huko Panama kwa ajili ya Genge la Medellín.

Hata mmoja wa viongozi wakuu wa genge hilo alidokeza kuwa Noriega alihusika moja kwa moja katika biashara hiyo haramu.

Kwa Maduro, utawala wa Trump unahusisha moja kwa moja kati boti zinazoenda kasi ambazo wamezipiga kwa mashambulizi ya anga katika bahari ya Caribbea na Maduro mwenyewe.

Tuhuma za Washington dhidi ya Maduro ni kwamba anaongoza kundi la Cartel of the Suns, ambalo linadaiwa kuwajumuisha wanajeshi wa sasa na wa zamani wa baraza kuu la kijeshi la Venezuela.

Lakini wachambuzi wengi wa vita vya dawa za kulevya wanahoji kama Cartel of the Suns ni kundi rasmi la wahalifu au ni muungano dhaifu wa maafisa mafisadi ambao wamejitajirisha kutokana na usafirishaji haramu wa dawa za kulevya na maliasili kupitia bandari za Venezuela.

Maduro na utawala wake wanakataa kuwepo kwa kundi lolote kama hilo, wakisema ni taarifa ya uongo isiyo na msingi inayosambazwa na Washington ili kumwondoa madarakani.

“Ghafla wameibua kitu kinachoitwa Cartel of the Suns,” alisema Waziri wa Mambo ya Ndani wa Venezuela, Diosdado Cabello. “Hawajawahi na hawataweza kamwe kuthibitisha uwepo wake kwa sababu halipo,” alisema mwezi uliopita.

Hata hivyo, kuna ushahidi wa biashara haramu ya dawa za kulevya ndani ya familia ya mke wa rais wa Venezuela.

Jamaa wawili wa Maduro walikamatwa nchini Haiti katika operesheni ya Marekani mwaka 2015. Ni watoto wa dada wa mke wa Maduro walikamatwa wakijaribu kuingiza kilo 800 za kokeni Marekani.

Francisco Flores de Freitas na Efrain Antonio Campo Flores walikaa miaka kadhaa gerezani Marekani kabla ya kurudishwa Venezuela mwaka 2022 kama sehemu ya kubadilishana wafungwa chini ya utawala wa Biden.

Utawala wa Trump sasa umewawekea vikwazo wawili hao pamoja na, Carlos Erik Malpica Flores.

Akitangaza vikwazo hivyo, Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent alisema: “Nicolás Maduro na washirika wake katika uhalifu nchini Venezuela wanaijaza Marekani dawa za kulevya zinazowatia sumu watu wa Marekani.

Ugaidi wa Dawa za Kulevya

k

Chanzo cha picha, Reuters

“Kundi la marafiki” ni lugha ambayo Washington iliitumia kuielezea serikali ya Noriega katika miaka ya 1980. Ripoti ya kamati ndogo ya Seneti ya Marekani wakati huo iliuita “utawala wa dawa za kulevya.”

Miaka 36 baadaye chini ya utawala wa Trump dhidi ya Maduro unatumia ya neno “ugaidi wa dawa za kulevya.”

Ni kauli yenye utata kwa sababu ya upana wake wa kisheria. Mapema mwaka 1987, Wizara ya Sheria ya Marekani ilifafanua ugaidi wa dawa za kulevya kama “ushiriki wa mashirika ya kigaidi na makundi ya waasi katika biashara haramu ya dawa za kulevya.”

Katika muktadha wa Venezuela, utawala wa Trump unasema uko katika vita dhidi ya magenge ya dawa za kulevya na umehalalisha mashambulizi yake dhidi ya boti zinazodaiwa kuwa na dawa kulevya huko Caribbea.

Pentagon inasema boti hizo ni shabaha halali. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, maswali mazito yameibuka kuhusu shambulizi la pili kwenye boti inayodaiwa kuwa ya dawa za kulevya Septemba 2, ambapo manusura wawili kutoka shambulizi la awali waliuawa.

Utawala wa Trump umejitetea dhidi ya madai kwamba shambulio la pili lilikuwa ni sawa na mauaji ya kiholela. Hata hivyo, suala hilo halijaisha na kuna wito kutoka kwa wabunge wa Marekani kutaka video yote iwekwe hadharani.

k

Chanzo cha picha, Trump

Hadi sasa, Pentagon haijachapisha video hiyo au ushauri wa kisheria kuhusu shambulio la pili, lakini Ikulu ya White House inasisitiza lilifanywa “kwa mujibu wa sheria za mapambano.”

Mvutano kati ya Marekani na Venezuela unaendelea kuongezeka na kuzidi, hasa kufuatia kukamatwa kwa meli ya mafuta ghafi ya Venezuela na vikosi vya Marekani.

Trump anasema baada ya Marekani kuchukua udhibiti wa anga na bahari ya Venezuela, kilichobaki ni kudhibiti ardhi. Wengi wanatamani kuona suluhu ya kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *