
Wanaongeza heshima nyingine baada ya pia kushinda Ballon d’Or ya wanaume na wanawake mwaka huu.
Dembélé alinga’a akiwa na Paris Saint-Germain, akiisaidia klabu hiyo kushinda taji lake la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku Bonmatí akitamba na Uhispania pamoja na FC Barcelona.
Tuzo za FIFA hupigiwa kura na manahodha wa timu za taifa, makocha, wanahabari na mashabiki kutoka kote duniani.
Katika kipengele cha makocha, Sarina Wiegman aliiongoza England kutwaa taji lake la pili mfululizo la Euro ya wanawake nchini Uswisi, wakati Luis Enrique aliiongoza PSG kushinda Ligi ya Mabingwa na ubingwa wa Ufaransa.
Tuzo nne kuu zilikuwa na orodha ileile ya washindi kama Ballon d’Or zilizotolewa Septemba mjini Paris. Sherehe za FIFA Best Awards zilifanyika Doha katika hafla ya faragha ya chakula cha jioni. Kisha kukawa na mechi ya Kombe la Mabara kati ya PSG na Flamengo.