Chanzo cha picha, Getty Images
Muda wa kusoma: Dakika 3
Manchester United na Roma ziko mbali sana katika tathmini ya thamani ya Joshua Zirkzee, 24, ambapo klabu hiyo ya Ligi Kuu England inataka ada ya takribani pauni milioni 35 na haijasema kama iko tayari kumruhusu mshambuliaji huyo wa Uholanzi aende kwa mkopo. (Corriere dello Sport)
Barcelona wana nia ya kuongeza mkataba wa kocha Hansi Flick hadi mwaka 2028, licha ya kocha huyo Mjerumani mwenye umri wa miaka 60 kusaini mkataba mpya na mabingwa wa Hispania hadi 2027 mwezi Mei mwaka huu. (Bild)
Barcelona pia wanawafuatilia beki wa Hispania wa Aston Villa, Pau Torres mwenye umri wa miaka 28, pamoja na beki wa Ujerumani wa Borussia Dortmund, Nico Schlotterbeck (26), wanasaka kusajili beki wa kati anayecheza upande wa kushoto. (ESPN)
Chanzo cha picha, Getty Images
Kipaumbele cha Chelsea katika majira ya joto kitakuwa kuimarisha kiungo wa kati, huku majina ya wachezaji wa England Kobbie Mainoo (20) wa Manchester United na Adam Wharton (21) wa Crystal Palace yakitajwa. (Telegraph)
Crystal Palace wanasaka beki wa kulia wa pembeni (right wing-back) katika dirisha la usajili la Januari baada ya jeraha la Daniel Munoz, ambalo linaweza kumuweka nje kwa muda mrefu mchezaji huyo wa Colombia mwenye umri wa miaka 29. (Sky Sports)
Miongoni mwa mabeki wa pembeni wanaoivutia Palace ni Sacha Boey wa Bayern Munich, beki wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 anayetarajiwa kuondoka klabu hiyo ya Bundesliga mwezi ujao. (Standard)
Kocha wa Palace Oliver Glasner anaamini kuwa beki wa England Marc Guehi (25) atamaliza mkataba wake kwa kubaki klabuni hadi mwisho wa msimu. (Standard)
AC Milan wako kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Niclas Fullkrug (32) kutoka West Ham, baada ya kupendekeza kumchukua kwa mkopo wenye kipengele cha kununua kwa usajili wa kudumu baadaye. (Bild)
Chanzo cha picha, Getty Images
Ole Gunnar Solskjaer aliishauri Manchester United kuwasajili Erling Haaland, Jude Bellingham na Declan Rice alipokuwa kocha Old Trafford, lakini badala yake klabu ilisajili Donny van de Beek, Jadon Sancho na Cristiano Ronaldo. (Mail)
Leeds United hawatarajiwi kutumia takribani pauni milioni 25 kumsajili mshambuliaji wa AC Milan na Mexico Santiago Gimenez (24), na badala yake wataangalia dili la mkopo wa muda mfupi kwa mshambuliaji mpya katika dirisha la Januari. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Ujerumani Nick Woltemade alikuwa chaguo la Bayern Munich majira ya joto kabla ya kujiunga na Newcastle United kutoka Stuttgart, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amesema kuwa, “kwa kuangalia nyuma, ninafurahi mambo yaliishia hivi.” (Sport Bild, via Sky Sports Germany)
Kiungo wa England wa Newcastle United, Alfie Harrison (20), ambaye bado hajacheza mechi ya kwanza ya timu ya wakubwa tangu ajiunge kutoka Manchester City mwaka jana, anavivutia vilabu vyaChampionship. (Sky Sports)