Gazeti la Al-Akhbar limeandika katika ripoti yake kwamba, kuongezeka kwa mashinikizo ya kisiasa ya Marekani dhidi ya Baghdad kumeufanya mchakato wa kuunda serikali mpya ya Iraq kuwa tata zaidi.

Gazeti la Al-Akhbar limeatangaza kuwa, kuongezeka mashinikizo ya kisiasa na kidiplomasia ya Marekani dhidi ya Baghdad yameufanya mchakato wa kuunda serikali mpya ya Iraq kukabiliwa na utata.

Mashinikizo haya ambayo yamepigiliwa msumari na kauli kali za Mark Sawaya, mjumbe wa Rais wa Marekani katika masuala ya Iraq, dhidi ya makundi ya muqawama, halijaongeza tu mkanganyiko wa mirengo ya kisiasa, bali pia yameleta radiamali ya wazi kutoka kwa makundi haya. Sawaya alitaja uwepo wa makundi ya muqawama kuwa upo nje ya mfumo wa serikali na akauona kuwa ni sababu ya kudhoofisha mamlaka ya kujitawala na uchumi wa Iraq.

Msimamo huu wa kuingilia mambo ya nchi zingine unaonekana kama sehemu ya shinikizo kubwa kutoka Washington, ambalo limeambatana na maonyo kuhusu kulinda miundombinu, kuhodhiwa silaha na serikali, na kuushurutisha uungaji mkono wa kimataifa na utambulisho wa serikali ijayo.

Mohammed Shia’ al-Sudani, Waziri Mkuu anayemaliza muda wake

Katika radiamali yake, chanzo kimoja katika makundi ya muqawama kimesisitiza kwa vyombo vya habari kwamba, makundi haya na harakati ya Hashd al-Sha’abi pamoja na washirika wao, ni sehemu muhimu ya mlinganyo wa kisiasa wa Iraq, wakiwa na angalau viti 97 bungeni, na kwamba vitisho vya kidiplomasia vya Marekani havitakuwa na natija yoyote ya maana kwao.

Ndani ya Iraq, mashinikizo haya yameufanya kuwa mgumu zaidi mchakato wa kuchagua Waziri Mkuu kwa muungano mkubwa wa “Fremu ya Uratibu wa Mashia”. Viongozi wa muungano wametangaza kwamba, dhamira yao ya sasa ni “nyeti sana” na kwamba lazima wamchague Waziri Mkuu ambaye anaitikia matakwa ya ndani na kudumisha uhusiano mzuri na ulimwengu wa nje. Mkazo ni juu ya “sifa” za waziri mkuu ajaye ambaye anapaswa kuwa, mtu asiye wa mzozo ambaye anaweza kupunguza wasiwasi wa kigeni bila kudhuru uhuru na mamlaka ya kitaifa.

Wapiganaji wa harakati ya Hash al-Shaabi

Weledi wa mambo wanaamini kwamba, kauli za maafisa wa Marekani ni sehemu ya mkakati mpana wa Washington wa kufafanua upya jukumu la makundi ya muqawama kupitia mashinikizo ya kisiasa na kiuchumi ya hatua kwa hatua. Lengo ni kutwisha uongozi wa kisiasa ambao unaweza kusimamia kesi ya makundi haya kutoka ndani ya mfumo, kwa sababu Marekani inafahamu kwamba, haiwezi kutumia nguvu kuyapokonya silaha makundi hayo.

Katika hali hii, makundi ya muqawama yametangaza sharti lao kuu la kuchaguliwa kwa waziri mkuu huru, asiye na uhusiano na chama chochote ambaye anawakilisha vipengele vyote vya kitaifa vya Iraq, na wameonya kwamba tishio lolote dhidi ya Iraq litakabiliwa na jibu la haraka, kwa sababu muqawama uko macho kila wakati na jaribio lolote la kuondoa jukumu lake, iwe ni la Marekani au utawala wa Kizayuni na kwamba, hilo litakabiliwa na majibu makali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *