Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeshiriki na kushinda tuzo ya Ubora katika Uhamasishaji Biashara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Uchumi.

Tuzo hizo za sekta ya umma zilizotolewa hivi karibuni jijini Dar es Salaam zinaangazia ubunifu unaofanywa na taasisi mbalimbali za umma, kwa muktadha wa kutoa huduma bora zinazoakisi maendeleo endelevu ya uchumi wa Tanzania.

TanTrade imekua ikifanikisha hayo kupitia Maonyesho ya Bishara ya Kimataifa, maarufu  Sabasaba, kuratibu maonyesho mbalimbali ya kimataifa kama vile Expo’s, mifumo mbalimbali ya kidijitali ya biashara kama vile Trade Portal, Biashara App, nk. Hafla ya  utoaji tuzo hizo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *