Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Prof. Peter Msoffe, amewataka wadau wa sekta binafsi kuchangamkia biashara ya kaboni kutokana na fursa nyingi zilizopo, akieleza kuwa Tanzania bado iko nyuma katika biashara hiyo.

Profesa Msoffe amesema hayo katika mkutano wa wadau wa maendeleo na mazingira uliofanyika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupokea taarifa ya mrejesho wa mkutano wa 30 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi (COP30).

#AzamTVUpdates
✍Rebeca Mbambela
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *