Bodi ya klabu ya Simba imekutana leo Desemba 18 katika kikao kilichoendeshwa na mwenyekiti wake Cresentius Magori hata hivyo bado klabu hiyo haijatoa taarifa ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikao hicho huku suala la kusuka benchi jipya la ufundi ni miongoni mwa mambo yanayodhaniwa kujadiliwa.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii Msemaji wa klabu hiyo Ahmed Ally amewasihi mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu na kusubiri matokeo ya kazi inayoendelea kufanywa na viongozi.

“Viongozi wetu makini wakiendelea na vikao madhubuti kwa ajili kuijenga Simba yetu, Niwaombe Wana Simba tuwaombee Viongozi wetu waweze kutenda yaliyomema kwa maslahi ya klabu yetu na tuwaunge mkono waweze kutimiza malengo ya kuijenga Simba imara” Ameandika Ahmed Ally.

Ameongeza kuwa Jambo la msingi sasa ni umoja na mshikamano, akiwahimiza mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba kuacha malumbano kwani hayasaidii badala yake wawekeze nguvu ya pamoja kuisaidia klabu yao.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *