Mashindano ya pooltable yajulikanayo kama Wakali wa Pooltable Msimu wa Pili yameanza rasmi leo tarehe 18 Disemba 2025, katika Ukumbi wa Skylight HQ Arena, uliopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yanashirikisha vilabu 12 pamoja na wachezaji Mmoja Mmoja, Wakiwemo Wakongwe na Wanawake, ambapo jumla ya takribani wachezaji 121 wanachuana kuwania ubingwa wa michuano hiyo.
Vilabu vinavyoshiriki ni pamoja na Sniper, Shooters, Skylight, Cue Master International, Cue Master Arusha, Moro Finest, Manyara, Marioo, Tiptop na Kijichi All Star, Legend Club, Worriors Pool Club huku ushindani mkali ukitarajiwa katika msimu huu wa pili.
Mashindano ya Wakali wa Pooltable yanalenga kukuza mchezo wa pooltable, kuibua vipaji na kuongeza ushindani miongoni mwa wachezaji nchini.
#StarTvUpdate