Rais wa zamani wa Ecuador Rodrigo Borja amefariki Alhamisi, Desemba 18, akiwa na umri wa miaka 90, Rais Daniel Noboa ametangaza kwenye mitandao ya kijamii.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Akiwa madarakani kati ya 1988 na 1992, Bw. Borja alitoa hati miliki za ardhi kwa takriban hekta milioni moja za ardhi kwa makundi ya watu wa kiasili kufuatia uasi wa kwanza wa watu wa kiasili nchini humo. Ilikuwa “mara ya kwanza” serikali kutoa ardhi kwa jamii hizi, Bw. Borja alikumbusha katika mahojiano ya mwaka 2019 na shirika la habari la AFP.

“Rodrigo Borja atabaki milele katika kumbukumbu ya Ecuador. Leo, nchi hii inatoa heshima kwa urithi wake,” Rais Daniel Noboa ameandika kwenyemtandao wa kijamii wa X, bila kutaja chanzo cha kifo chake.

Serikali ya Bw. Borja ilifanikiwa kuwaondoa watu kutoka kundi la msituni la AVC (Alfaro Vive Carajo) na iliendeleza kampeni ya kusoma na kuandika na usambazaji wa kifungua kinywa shuleni. Mapema maishani mwake, alifungwa gerezani wakati wa masomo yake ya chuo kikuu kwa kupinga serikali ya mhafidhina José María Velasco Ibarra.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *