Mwanzilishi wa WikiLeaks, Julian Assange, amewasilisha kesi ya jinai dhidi ya Taasisi ya Nobel huko Sweden kufuatia uamuzi wa taasisi hiyo wa kutoa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa kiongozi wa upinzani wa Venezuela, Maria Corina Machado.
Taarifa iliyochapishwa na WikiLeaks kwenye mitandao ya kijamii imesema: Tuzo ya mwaka huu ya Nobel ni kielelezo cha “ubadhirifu mkubwa” wa fedha na “uwezeshaji wa uhalifu wa kivita” chini ya sheria ya Sweden.
Assange anawashutumu maafisa thelathini waliohusishwa na Taasisi ya Nobel kuwa wamebadilisha “chombo cha amani kuwa chombo cha vita.”
Kamati ya Nobel ilimpa Machado tuzo hiyo kwa madai ya kukuza haki za kidemokrasia na eti mapambano yake ya kuelekea kwenye haki na amani kutoka kwenye udikteta.
Hata hivyo mwasisi wa WikiLeaks, Julian Assange ameashiria uungaji mkono wa Machado kwa kampeni inayokiuka sheria za kimataifa ya Rais wa Marekani, Donald Trump ya miezi kadhaa dhidi ya Rais wa Venezuela mwenye msimamo wa mrengo wa kushoto, Nicolas Maduro.
Mwanzilishi wa WikiLeaks amesema kwamba kuchaguliwa Maria Corina Machado kwa ajili ya Tuzo ya Amani ya Nobel kumekiuka wosia wa Alfred Nobel wa mwaka 1895—ambao unaeleza kwamba tuzo hiyo inapaswa kutolewa kwa mtu ambaye amefanya “kazi bora zaidi kwa ajili ya udugu miongoni mwa mataifa, kwa ajili ya kukomesha au kupunguza mizozo ya kivita, na kwa ajili ya kuitisha na kukuza mikutano kwa ajili ya amani”
Maria Corina Machado ni muungaji mkono wa utawala katili wa Israel na ameahidi kupeleka ubalozi wa Venezuela huko Quds Tukufu inayokaliwa kwa mabavu iiwapo atashika madaraka nchini Venezuela.

Kinyume na sera za Machado, Mnamo 2009, Venezuela, chini ya uongozi wa Hugo Chavez, na kiongozii wa sasa wa nchi hiyo, Nicolas Maduro ilikata uhusiano wa kidiplomasia na Israel na kumfukuza balozi wa utawala huo haramu ikipinga vita vya Israel dhidi ya watu wa Gaza vya 2008-2009.
Rais wa Marekani, ambaye mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Maria Corina Machado, alimkabidhi tuzo yake, ametuma meli kubwa za kivita katika Bahari ya Karibi akitishia kuishambulia Venezuela, na hadi sasa majeshi ya Marekani katika eneo hilo yameua watu karibu mia moja.