
Virusi vya Ukimwi au VVU huenezwa kwa njia ya kuongezewa damu, kuwa na jeraha la wazi au michubuko na kugusana na damu au maji maji ya mwilini ikiwamo ya sehemau za siri yenye maambuki-zi wakati wa kujamiana.
VVU vinaweza kuwapo kwa kiasi kidogo sana katika machozi na mate. Ili kuambukizwa kwa njia ya ma-te, itahitajika kumeza mate kiasi cha lita mbili.
Maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto hutokea wakati wa ujauzito, uchungu, kujifungua na kunyonyesha.
Kuchangia vitu vyenye ncha kali kama vifaa vya kunyolea, kutogea masikio na pua na kuchorea tatuu huchangia maambukizi kwa asilimia 2-4
VVU huitaji kujipachika kwenye vipokezi vya seli nyeupe ili kuweza kuingia ndani ya seli hizo, in-aposhindikana huvitaweza kujidurufisha na kuongezeka idadi.
Endapo vitafanikiwa kuingia na kujidurufisha, huendelea kuvamia seli kinga zingine maelfu kwa maelfu.
Hii husababisha kinga kushuka hatimaye mwili kushindwa kujilinda dhidi ya magonjwa nyemelezi kama vile kifua kikuu, nimonia kali na saratani ya ngozi na uambukizi katika ubongo.
Vipimo vya kawaida vya haraka vinaweza kubaini VVU baada ya wiki mbili tangu kupata maambukizi, dalili za awali zinaweza kujitokeza baada ya wiki 2-4 tangu kuambukizwa.
Matumizi ya mipira yaani condoms yanasaidia kupunguza kasi ya maambukizi, lakini usahihi wa uvaaji na kuitumia usipofuatwa unaweza kupata maambukizi.
Ni kweli matumizi ya kupaka mafuta au vilainishi yanapunguza hatari ya kupata michubuko lakini bado haizuii moja kwa moja kugusana na damu na maji maji yenye VVU.
Mbinu ya kuosha sehemu za siri kwa maji mengi na sabuni si njia sahihi ya kuzuia VVU, bali ni njia bora kwa ajili ya usafi na kuzuia baadhi ya vimelea lakini si VVU.
Kujamiana kinyume na maumbile kuna hatari ya kuambukizwa VVU kirahisi, hii ni kutokana na njia hiyo kupata michubuko kirahisi.
Watumiaji wa dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga wanaambukizwa VVU kwa kushirikiana vifaa vya kujifungua ikiwamo sindano.
Ni kweli mbu hueneza malaria lakini hawezi kueneza VVU kwa kumng’ata mwathirika wa VVU na hii ni kwasababu anapofyonza damu humpa mate anayemng’ata na wala hampi damu.
Vile vile mfumo wake wa chakula hauwezeshi virusi kuishi na huku pia vimeng’enya vyake huviua vi-rusi. Vile vile hata wadudu kama kunguni, nzi na mbung’o hawawezi kueneza VVU.
Ukimwi hauna tiba wala kinga, isipokuwa zipo dawa za kufubaza makali ya virusi (ARVs) ambazo ndizo zimesaidia kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Kuanzia kutumika sindano ya kufubaza makali ya VVU ijulikanayo Lenacapavir itapunguza kadhia ya kumeza vidonge vya ARVs kila siku.
Sindano hii imeidhinishwa kama kingatiba ya muda mrefu kabla ya maambukizi kitabibu PrEP, kwa ajili ya wale walio katika hatari zaidi ya kupata maambukizi.
Endapo dawa za ARVs zikitumika vizuri, kiwango cha virusi huwa chini kabisa kiasi cha kutoweza kuam-bukiza wengine. Ndio maana wapo wenza wanaoishi huku mmoja akiwa na VVU.
Matumizi ya pombe na dawa za kulevya yanachochea tabia hatarishi iikiwamo kufanya ngono zembe, hivyo kuhatarisha kupata maambukizi kirahisi.
Duniani kuna mamilioni ya watu ambao bado hawajui hali zao za kiafya. Hivyo epuka unyanyapaa na ubaguzi kwa wagonjwa wanaoishi na VVU, inashauriwa kupima na kujua hali yako.