Katika kile kinachoonekana wazi kuwa ni madhara ya uchafuzi wa mazingira na mvurugiko wa hali ya hewa kutokana na uharibifu mkubwa wa hewa unaofanywa na madola ya viwanda duniani, taarifa kutoka Morocco zinasema kuwa, nchi hiyo ya jangwa imekumbwa na mawimbi makubwa ya baridi kali ambayo hayajawahi kutokea.

Vyombo vya habari vya ndani na nje ya Morocco vimeripoti kuwa, nchi hiyo ya kaskazini magharibi mwa Afrika imekumbwa na wimbi la baridi kali linaloathiri maeneo kadhaa ya nchi hiyo ya kifalme hasa maeneo ya milimani na ya bara.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, nyuzijoto zimeshuka sana na kufikia hata kunyesha theluji katika maeneo ya miinuko, na kusababisha hali kuwa ngumu kwa wakazi wa maeneo hiyo na watumiaji wa barabara ambao hawana mazoea na hali hiyo ya hewa.

Mamlaka husika zimetangaza kuwa, zimeongeza kiwango cha kuhamasisha watu kote nchini humo ili wajitokeze kuzisaidia jamii zilizoathiriwa na baridi kali na kuhakikisha njia zinafunguliwa na vyombo vya barabarani vinaendelea na safari zake kama kawaida.

Juhudi hizo zinalenga pia kutoa msaada kwa wakazi wanaoishi katika mazingira magumu. Timu za dharura zimetumwa kusafisha barabara zilizofunikwa na theluji na kufuatilia hatari zinazohusiana na hali ya hewa.

Watu wamehimizwa kuchukua tahadhari sana kwani kipindi cha baridi kali kinatarajiwa kuendelea pia katika siku zijazo. Mamlaka husika zinasema kuwa zinaendelea na jitihada zao za kupunguza athari za hali mbaya ya hewa.

Morocco ni nchi ya jangwa. Inahesabiwa kuwa ni nchi ya tatu zenye jangwa kubwa zaidi duniani. Jangwa la Morocco lina ukubwa wa zaidi ya kilomita mraba 9,400,000. Morocco inahesabiwa kuwa ni nchi ya joto, na ingawa kuwa na hali ya hewa kama hiyo kuna faida zake lakini pia huja na changamoto nyingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *