Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Reuben Kwagilwa, amepata ajali majira ya saa tisa usiku katika wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma.

Ajali hiyo imetokea wakati Mhe. Kwagilwa akiwa safarini akitokea mkoani Mbeya ambako alihudhuria ziara ya Waziri Mkuu, na kuelekea mkoani Lindi kwa ajili ya kuungana na ziara nyingine ya Waziri Mkuu,Dkt. Mwigulu Nchemba.

Tunafuatilia kwa karibu tukio hili na tutatoa taarifa zaidi kadri zinavyopatikana kutoka kwa maafisa wa Serikali na vyombo vya usalama vilivyoko eneo la tukio

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *