#HABARI: Mtandao wa kijamii wa TikTok umefikia makubaliano ya kuanzisha ubia na kampuni ya Marekani, hatua inayolenga kutimiza masharti ya mamlaka na hivyo kuepuka marufuku ya matumizi nchini humo.

TikTok, kwa kushirikiana na kampuni mama yake ya China, ByteDance, imeunda ubia huo pamoja na kampuni za Oracle na Silver Lake, sambamba na mfuko wa uwekezaji wa Falme za Kiarabu unaojulikana kama MGX.

Kampuni mpya, itakayojulikana kama TikTok USDS Joint Venture, itakuwa chini ya udhibiti mkubwa wa wawekezaji wa Marekani na itahusika na usimamizi wa usalama wa data na masuala ya usalama wa taifa.

Kwa mujibu wa TikTok, mtandao huo una jumla ya watumiaji wapatao milioni 170 nchini Marekani.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *