Mnamo siku ya Jumatano, Bunge la Marekani liliondoa vikwazo vilivyoilenga Syria chini ya utawala wa Bashar al-Assad ambaye aliondolewa madarakani mwezi Desemba mwaka jana.

Sheria ya Caesar, iliyopewa jina la mpiga picha asiyejulikana na aliyefichua ukatili katika magereza ya Assad, ilizuia kwa kiwango kikubwa uwekezaji na kuiondoa Syria kutoka kwenye mfumo wa kimataifa wa benki.

Katika taarifa yake, wizara ya mambo ya nje mjini Damascus imesema “imeikaribisha” hatua hiyo, ikiitaja kuwa “mlango wa kuingia katika awamu ya ujenzi upya na maendeleo” nchini humo.

Wizara hiyo pia imetoa wito kwa raia wote wa Syria waliomo nchini na nje ya nchi kuchangia katika juhudi za kulijenga upya taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *