Wakulima 40 wa mbegu kutoka katika Halmashauri sita za Mkoa wa Simiyu, wamepewa elimu ya namna ya uzalishaji wa mbegu bora zenye tija zitakazo wawezesha Wakulima wa mazao mbalimbali mkoani humo kupata mazao kwa wingi kupitia mbegu hizo, huku Wakulima hao wakiomba kujengwa kwa mabwawa yatakayo saidia umwagiliaji na kuacha kutegemea mvua peke.