Katika kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka wananchi mkoani Manyara wametakiwa kusherehekea kwa amani na utulivu lakini kujiandaa pia kupeleka watoto shule ifikapo mwezi januari ambao wanastahili kuanza ďarasa la kwanza na hata wanaorudi shuleni na wale wa kidato cha kwanza.
Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga wakati akitoa Salam za mwisho wa mwaka kwa na kuwatakia heri ya sikukuu wananchì mkoani hapo.
Sendiga pia amesema kuelekea sikuku hiźo serikali imejiandaa kikamilifu kuimarisha amani na utulivu wakati wote wa sherehe hizo kutokana na ongezeko la watu wanaorudi maeneo yao ya asilì kuungana na ndugu jamaa na marafiki zao kwaajili ya sikukuu hizo.
Pia amewetaka wazazi kuchukua tahadhari ya kutoka na watoto kwene maeneo ya starehe iwapo hakuna ulazima wasitoke nao kuepuka usumbufu unaoweza kutokea kwao