#HABARI: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo hadi Desemba 30, 2025, baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kusoma maelezo ya mashahidi na vielelezo. Wakili wa Serikali, Glory Kilawe, ameeleza mbele ya Hakimu Geofrey Mhini kuwa uamuzi huo umetokana na kubainika kuwa baadhi ya nyaraka muhimu hazikuwepo kwenye mfumo wa mahakama, hivyo kuhitaji muda wa kufanya marekebisho.
Katika shauri hilo, wafanyabiashara sita akiwemo Lendela Mdete na wenzake, wanakabiliwa na shtaka la mauaji bila kukusudia kufuatia tukio lililotokea Novemba 16, 2024, katika mitaa ya Mchikichi na Kongo. Washitakiwa hao wanadaiwa kushindwa kutimiza majukumu yao, jambo lililosababisha kuporomoka kwa jengo hilo na kupelekea vifo vya watu 31, wakiwemo Said Juma na Elizabeth Mbaruku.
Wakati kesi hiyo ikisubiriwa kuendelea, upande wa Jamhuri umebainisha kuwa unatarajia kuwasilisha jumla ya mashahidi 55 na vielelezo 54 ili kuthibitisha mashtaka hayo. Washitakiwa wataendelea kusubiri hadi tarehe hiyo mpya ya Desemba 30 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya kina ya ushahidi dhidi yao.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.