Mo Salah

Chanzo cha picha, BBC Sport

Muda wa kusoma: Dakika 4

Uhusiano kati ya nyota Mohamed Salah na Liverpool unaweza kuwa unapitia misukosuko, lakini hakuna anayeweza kutilia shaka mafanikio yake makubwa akiwa na klabu hiyo yenye maskani yake Anfield.

Nyota huyo wa Misri ameshinda mataji mengi akiwa na Liverpool, lakini bado hajawahi kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) akiwa na timu yake ya taifa.

Ingawa ana nafasi ya kubadilisha historia hiyo kwenye fainali ijayo itakayofanyika Morocco, wapo baadhi ya wachezaji wakubwa kabisa katika historia ya soka Afrika ambao walimaliza soka lao bila kutwaa taji hili kubwa zaidi barani Afrika.

BBC inakuletea majina matano makubwa ambayo hayakuwahi kushinda AFCON.

Mohamed Salah (Misri)

Maxamed Saalax

Chanzo cha picha, Getty Images

Je, mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 33 ataiongoza timu yaake ya taifa ya Misri wakati huu? Misri ndiyo timu yenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya AFCON, ikiwa na mataji saba.

Hata hivyo, hawajashinda taji lolote tangu mwaka 2010, kipindi ambacho Salah ndiyo ameibukia.

Ikumbukwe kuwa Misri haikufuzu AFCON za 2012, 2013 na 2015, jambo lililomfanya Salah kucheza AFCON yake ya kwanza mwaka 2017, mashindano waliopoteza dhidi ya Cameroon.

Salah, aliyeshinda tuzo ya Mchezaji Bora Afrika mwaka 2017 na 2018, alipata pigo lingine mwaka 2019 wakati AFCON ilipofanyika nchini Misri. Timu ya Afrika Kusini iliwaondoa kwenye raundi ya 16.

Misri ilirejea fainali ya AFCON 2021, lakini Salah alipoteza dhidi ya nyota mwenzake wa Liverpool wakati huo, Sadio Mané. Salah alipangwa kupiga penati ya tano ya kuamua mshindi, lakini hakupata nafasi hiyo kwani Senegal walishinda penati 4–2 kabla haijafikia zamu yake.

Didier Drogba (Ivory Coast)

Ciyaaryahan qiimo weyn dunida ku leh

Chanzo cha picha, Getty Images

Drogba alikuwa mchezaji wa mechi kubwa, akijulikana kwa mafanikio yake akiwa na klabu ya Chelsea akifunga mabao tisa katika fainali 10 kubwa walizocheza, na kushinda nane kati ya hizo.

Hata hivyo, katika mashindano ya AFCON, bahati haikuwa upande wake.

Mwaka 2006, Ivory Coast walipoteza fainali dhidi ya wenyeji Misri kwa mikwaju ya penati 4–2, Drogba akishindwa kufunga penati yake.

Mwaka 2012, walirejea tena fainali wakiwa wanapewa nafasi kubwa dhidi ya Zambia, lakini tena wakapoteza, na Drogba kushindwa kuleta tofauti.

Licha ya kushinda kila kitu kwenye soka la klabu na hata kuchangia kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ivory Coast, taji la AFCON lilibaki ndoto kwa Drogba.

George Weah (Liberia)

Xulka dalkiisa Liberia labo jeer oo kaliya ayey ka qeybgaleen tartanka, labadaasna isaga ayaa ka mid ah ciyaartoyda, mana u suuragelin in uu qaado koobka.

Chanzo cha picha, Getty Images

Liberia imeshiriki AFCON mara mbili tu, na Weah alikuwa sehemu ya kikosi katika mashindano yote mawili bila mafanikio.

Kwa upande wa mafanikio binafsi, Weah ni mmoja wa wachezaji wakubwa zaidi Afrika.

Yeye ndiye Mwafrika pekee aliyewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya Ballon d’Or, mwaka 1995, na pia alichaguliwa Mchezaji Bora Afrika mwaka huo huo.

Liberia ilicheza AFCON kwa mara ya kwanza mwaka 1996, lakini ikatolewa hatua ya makundi. Walirejea tena mwaka 2002 bila mafanikio.

Baada ya soka, Weah aliingia kwenye siasa na kuwa Rais wa Liberia kuanzia 2018 hadi 2024.

Nwankwo Kanu (Nigeria)

Kanu

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji mwenye akili na mtulivu mwenye uwezo wa kipekee, Kanu alikuwa na mafanikio makubwa katika soka la klabu, akishinda Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Ajax na Kombe la UEFA akiwa na Inter Milan.

Katika soka la kimataifa, alishinda Kombe la Dunia la U-17 mwaka 1993 na dhahabu ya Olimpiki mwaka 1996.

Fursa yake kubwa ya kushinda AFCON ilikuwa mwaka 2000, lakini Nigeria walipoteza fainali dhidi ya Cameroon kwa mikwaju ya penati.

Kanu alishinda tuzo ya Mchezaji Bora Afrika mara mbili, lakini alimaliza soka lake akiwa na medali za fedha na shaba pekee za AFCON.

Michael Essien (Ghana)

Ghana haijashinda AFCON tangu mwaka 1982, jambo lililosababisha vizazi vingi vya wachezaji wakubwa kukosa taji hilo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Ghana haijashinda AFCON tangu mwaka 1982, jambo lililosababisha vizazi vingi vya wachezaji wakubwa kukosa taji hilo.

Essien, anayechukuliwa kama kiungo bora zaidi katika historia ya Ghana, alikuwa miongoni mwao. Kama Drogba, alishinda mataji mengi akiwa na Chelsea kati ya mwaka 2006 na 2012.

Mwaka 2008, Ghana walipokuwa wenyeji wa AFCON, Essien alitajwa miongoni mwa wachezaji bora wa mashindano, lakini Cameroon waliwaondoa kwenye nusu fainali.

Ingawa alicheza mechi nyingi kwa taifa lake, majeraha ya mara kwa mara yalizuia uwezo wake kamili kung’ara na ndoto ya kutwaa AFCON ikafa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *