Bondia wa uzito wa juu wa Uingereza, Anthony Joshua, ametumia raundi sita pekee kumaliza pambano dhidi ya Jake Paul, bondia chipukizi na nyota wa Mtandao wa YouTube, ambaye alitumia muda mwingi kujilinda.

Pambano hilo lililomalizika asubuhi ya leo Desemba 20,2025 lilionekana  kuwa la tofauti zaidi katika historia ya ndondi duniani,Shirika la Habari la Uingereza linalojishughulisha na michezo BBC Sport  limeeleza.

Katika pambano hilo, Joshua (36), bingwa wa dunia mara mbili, ameonekana kukosa subira huku Paul akicheza kwa kukimbia ulingoni kwa muda mrefu, akikataa kupambana uso kwa uso na mpinzani wake.

Bondia Anthony Joshua akimuangalia mpinzania wake, Jake Paul baaada ya kumdondondosha kwa KO raundi ya sita pambano la uzito wa juu. Picha na Mtandao

 Hata hivyo, Joshua alimdhibiti mpinzani wake huyo kwa kumwangusha mara mbili katika raundi ya tano.

Paul aliangushwa tena katika raundi ya sita kabla ya Joshua kumpiga ngumi ya mkono wa kulia iliyomaliza pambano hilo ghafla katika ukumbi wa Kaseya Center jijini Miami.

Mmarekani huyo baada ya kuangushwa aliinuka na kuondoka ulingoni bila msaada.

Bondia Anthony Joshua akishangilia baada ya kumdondosha mpinzania wake kwa KO raundi ya sita katika pambano la uzito wa juu. Picha na Mtandao

“Haukuwa mchezo wangu bora. Lengo lilikuwa ni kumbana Jake Paul na kumuumiza. Ilichukua muda mrefu kidogo kuliko nilivyotarajia, lakini hatimaye ngumi ya kulia ilipata ilipokusudiwa,” amesema Joshua, mwenye umri wa miaka 36.

Matokeo hayo yalikuwa yametabiriwa kwa kiasi kikubwa na ulimwengu wa ndondi, huku pambano hilo tata likizua maswali kuhusu hatari za kiafya zinazotokana na tofauti kubwa ya uzoefu, ukubwa na nguvu kati ya wapiganaji.

Joshua alipata ushindi wake wa 29 katika mapambano 33 ya kulipwa na sasa anaweza kuelekeza mawazo yake kwenye pambano linalosubiriwa kwa muda mrefu dhidi ya Tyson Fury mwaka ujao.

Joshua aliingia ulingoni kwanza na kupokelewa kwa hisia mchanganyiko na mashabiki ndani ya ukumbi wenye viti 20,000.

Katika pambano hilo,kengele ya mwanzo ilipopigwa, Paul alianza kuzunguka ulingo akirudi nyuma, na muda mfupi baadaye kelele za kuzomewa zikasikika.

Joshua alimfuata akirusha ngumi kushoto na kulia ambazo mara nyingi zilikosa shabaha, kila kosa likisababisha mshangao kwa watazamaji.

 Paul alijibu kwa kutoa ulimi wake, akigeuza tukio kuwa la maigizo.

Nyota wa gofu Rory McIlroy, aliyekuwa ameshinda tu tuzo ya Sports Personality of the Year, alikuwapo kando ya ulingo pamoja na marapa Rick Ross na Timbaland.

Raundi ya tano ilileta kile ambacho wengi walikuwa wakitarajia mapema zaidi. Ngumi ya kulia ilimgusa Paul begani na kumwangusha chini.

Muda mfupi baadaye, ngumu zilizopigwa kwake mfululizo zilimuangusha tena .

Alisimama kwa shida, ngumi nyingine nzito ya kulia ilimpata katika raundi ya sita na kukuangusha tena Paul, na baadhi ya mashabiki wakaanza kumtaka mwamuzi kusitisha pambano.

Waliokumbuka knock-out kali ya Joshua dhidi ya bingwa wa zamani wa UFC Francis Ngannou mwaka uliopita walihisi mwisho kama huo ulikuwa unakaribia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *