
Shirika hilo la wakimbizi lenye makao yake makuu mjini Geneva nchini Uswisi, huwasaidia mamilioni ya watu kote duniani ambao wamelazimika kuzikimbia nchi zao kutokana na vita na madhila mbalimbali.
Uteuzi huo wa Salih mwenye umri wa miaka 65 ulifanyika siku ya Alhamisi, baada ya jina lake kupendekezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres na kuthibitishwa rasmi na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.
Rais huyo wa zamani wa Iraq anachukua uongozi wa shirika ambalo linakabiliwa na tatizo kubwa la ufadhili, huku idadi ya wakimbizi ikiongezeka zaidi kutokana na vita na migogoro nchini Ukraine, Afghanistan, DRC, Sudan na nchi nyingine nyingi.