
Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imejibu tangazo la Jumanne, Desemba 16, la kufunguliwa kwa uchunguzi wa kimahakama nchini Mali unaomlenga Yann Vezilier, ikielezea kukamatwa kwake kama hatua “isiyokubalika na ni kinyume cha sheria.”
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Afisa huyu wa idara ya ujasusi ya Ufaransa alikuwa akihudumu katika ubalozi wa Ufaransa nchini Mali, ambapo aliidhinishwa rasmi. Alikamatwa miezi minne iliyopita, mwezi Agosti, anachunguzwa na kitengo cha mahakama nchini Mali kinachobobea katika mapambano dhidi ya ugaidi kwa vitendo vilivyoelezewa kama “vitendo vinavyolenga kuhatarisha usalama wa taifa.”
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Ijumaa, Desemba 19, msemaji wa Quai d’Orsay (Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa) alidai kwamba mamlaka ya Ufaransa “haikuarifiwa kuhusu kukamatwa kwa afisa wake” na kwamba “haikuwa na idhini ya kibalozi kumfikia raia wao.”
Ufaransa pia inabainisha kwamba inaongeza juhudi zake kwa mamlaka huko Bamako ili kuhakikisha Yann Vezilier aachiliwa.
Habari zaidi zinakujia…