Rais wa Taiwan Lai Ching-te ameahidi siku ya Jumamosi, Desemba 20, uchunguzi wa kina kuhusu shambulio hilo lililogharimu maisha ya watu watatu siku kwenye kituo ha treni cha Taipei. Mshambuliaji aliyekuwa na kisu kikubwa na vilipuzi vya Molotov aliwatishia watu, pia akiwajeruhi watu wasiopungua 11.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mshukiwa huyo, mwanamume mwenye umri wa miaka 27, pia aliwajeruhi jumla ya watu 11, kulingana na idadi mpya iliyotolewa na polisi leo Jumamosi, kabla ya kujiua, kulingana na meya wa mji mkuu. Mwanamume huyo, akiwa na kisu, vinywaji vilipuzi vya Molotov, na mabomu ya moshi, alishambulia umma katika vituo viwili, ikijumuisha kituo cha treni cha kati, na duka kubwa la ununuzi.

Rais Lai Ching-te amesema aliamuru “uchunguzi kamili na wa kina” kuhusu tukio hilo na kuahidi “kuwapa umma maelezo kamili ya ukweli” kwa kuwatembelea waliojeruhiwa. “Nataka kutoa rambirambi zangu kwa wale waliopoteza maisha yao katika tukio la kusikitisha, shambulio la kutisha na la kikatili la jana usiku, na kutoa rambirambi zangu kwa familia zao,” alisema kutoka hospitalini.

Mkuu wa Polisi wa taifa Chang Jung-hsin amesema leo Jumamosi kwamba mshukiwa alitekeleza kitendo chake hicho kiovu peke yake. “Alifanya kitendo hicho kulingana na mpango wa kuwaua watu bila mpangilio. Kuhusu nia, nadhani bado inahitaji kuchunguzwa,” amebainisha. Siku ya Meya wa mji mkuu wa Taiwan Chiang Wan-an alisema kwamba mshukiwa, anayetafutwa kwa kukataa kuingia jeshini kwa lazima, inaonekana “alijiua kwa kuruka kutoka jengo ili kuepuka kukamatwa.”

Video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha mshukiwa akirusha mabomu ya moshi barabarani kabla ya kushambulia watu wengine na kuelekea kwenye duka la karibu la ununuzi huku akinyoosha kisu kirefu. Mamlaka imeongeza hatua za usalama kote Taiwan kufuatia tukio hilo. “Hivi sasa, maeneo yote makubwa, ikiwa ni pamoja na vituo vya treni, barabara kuu, vituo vya treni za chini ya ardhi, na viwanja vya ndege, yako chini ay uangalizi mkali,” waziri mkuu alisisitiza.

Uhalifu wa kikatili bado ni nadra nchini Taiwan. Hata hivyo, mwaka wa 2014, mwanamume mmoja alidunga kisu abiria kwenye treni ya chini ya ardhi ya Taipei, na kuwaua watu wanne. Aliuawa kwa mauaji hayo mwaka wa 2016.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *