
Angalau wakimbizi 40 wa Kongo wamefariki kutokana na kipindupindu na utapiamlo katika kambi ya mpito ya Gatumba nchini Burundi katika muda wa siku 10 pekee. Kifara Kapenda, naibu meya wa Uvira, ambaye pia ametafuta hifadhi katika mji mkuu wa kiuchumi wa Burundi, Bujumbura, tangu jiji la Uvira lilipoangukia mikononi mwa waasi wa AFC/M23, aliongoza mkutano na raia wa Kongo wanaoishi nje ya nchi siku ya Alhamisi, Desemba 18, ili kujadili mgogoro huo na kupata suluhu za muda.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mkimbizi katika kambi hiyo alielezea hali mbaya: ukosefu wa maji ya kunywa, chakula, dawa, na vifaa vya kujikimu, huku watoto na wanawake wengi wakiwa miongoni mwao, kulingana na Radio OKAPI.
Anasema kwamba “watu 8 walifariki Desemba 18 pekee, 5 zaidi siku moja kabla, na zaidi ya 40 kwa jumla katika muda wa siku 10, kutokana na kipindupindu na njaa.”
Wakimbizi hao wanaishi katika kambi za muda au kambi za mpito, na hivyo kuzidisha udhaifu wao.
Wito wa haraka wa msaada
Mkimbizi huyu, kama wengine wengi, anaomba serikali ya Kongo iingilie kati mara moja ili kupunguza kiwango cha vifo miongoni mwa watu hawa walio hatarini, waliokimbia shambulio la M23 dhidi ya mji wa Uvira.
Naibu meya pia anatoa wito kwa mamlaka ya Kongo na mashirika ya kibinadamu kuwasaidia watu 30,000 wa Kongo wanaopewa hifadhiwa katika mji wa Gatumba, Magharibi mwa Bujumbura. Kamati ya dharura imeundwa ili kuratibu juhudi za kuingia kati na kusambaza misaada.