#MICHEZO: Siku moja baada ya Simba kumtangaza Steve Barker mwenye umri wa miaka (57) kutoka Afrika Kusini kuwa Kocha wa Mkuu mpya, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Timu hiyo ya Simba Ahmed Ally, amesema baada ya kupatikana Kocha huyo mpya, Heshima imerudi kwenye timu hiyo ya wekundu wa Msimbazi.

Ahmed Ally ameandika ujumbe kwenye mtandao wake wa Kijamii wa Instagram ukisomeka hivi…’Huyu Kocha wetu mpyaaaa aaaah ana hatariii 😀😀 Acha nisiseme sanaaa ila heshima yetu imerudii’

Ifahamike tu kwamba Barker amejiunga na Simba akitokea Stellenbosch aliyoiongoza na kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita, ambapo katika msimu huu ameiongoza Stellenbosch katika michezo 24 ya mashindano tofauti, na kupata ushindi mara nane na kutoka sare sita na kupoteza mechi 10.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *