Ni desturi ya kale kwa Watanzania hususani wanaotoka mikoa ya Kaskazini mwa nchi kama Kilimanjaro na Arusha hukusanyika kwenye mikoa hiyo kila ifikapo mwishoni mwa mwaka.
Hali hii imebatizwa jina la ‘Kuhesabiwa’ ikiweka mkazo katika uwajibikaji wa watu wa ukanda huo kurejea vijijini kuwatembelea wazazi, ndugu, jamaa na marafiki na kufurahia pamoja Sikukuu za mwisho wa mwaka.
Je, unafikiri watu wanapokusanyika katika familia zao, koo huzingatia lengo gani? Msikilize mshauri wa masuala ya kijamii, Sialove Lukumay akizungumzia umuhimu wa watu kukusanyika.
✍Halima Abdallah
Mhariri | @moseskwindi
#AzamTVUpdates #hellowikiendi