Wajumbe wa Marekani, Ulaya na Ukraine pamoja na maafisa kadhaa wa kijeshi wanatarajiwa kuhudhuria mazungumzo hayo jimboni Florida, yatakayojikita katika masuala mawili muhimu ambayo ni hakikisho la usalama kwa Ukraine na hatma ya maeneo ya Ukraine yanayodhibitiwa sasa na Urusi.

Kulingana na pande zote, maendeleo chanya yamepatikana kuhusu suala la hakikisho la usalama baada ya kusainiwa makubaliano ya kusitisha mapigano, lakini rais wa  Ukraine  Volodymyr Zelensky amesema mazungumzo hayo yalikuwa yakitafuta namna ya kupata mkataba imara wa amani na wala si kuhusu masuala ya kugawana maeneo au rasilimali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *