
Chanzo kimoja cha usalama huko Syria kimesema mashambulizi hayo yalilenga maeneo ya kundi hilo katika eneo kubwa la jangwa la Badia nchini Syria ikiwa ni pamoja na majimbo ya Homs, Deir Ezzor na Raqa, na kwamba hayakujumuisha operesheni za ardhini.
Nchi jirani ya Jordan imethibitisha kushiriki katika operesheni hiyo ya Marekani , ambayo ni ya kwanza tangu kuangushwa kwa utawala wa Bashar al Assad Desemba mwaka jana, na imefanyika baada ya shambulio baya dhidi ya wanajeshi wa Marekani mwishoni mwa wiki iliyopita.
Vikosi vya Marekani vimesema vimeshambulia zaidi ya maeneo 70 ya kundi hilo, hatua iliyotajwa na Rais Donald Trump kuwa ni “kisasi madhubuti” kufuatia shambulio la Desemba 13 huko Palmyra lililowaua wanajeshi wawili wa Marekani na raia mmoja.