
Khan na mkewe walikana mashtaka hayo walipopandishwa kizimbani mwaka 2024. Walifunguliwa mashtaka ya kuuza zawadi hizo, ikiwa ni pamoja na vito kutoka kwa serikali ya Saudi Arabia, kwa bei ya chini kuliko thamani yake, wakati Khan alipokuwa madarakani.
Kulingana na sheria ya Pakistan, ili maafisa wa serikali na wanasiasa waweze kumiliki zawadi zilizotolewa na viongozi wa kigeni, ni lazima wazinunue kwa thamani ya bei ya soko na kutangaza mapato yoyote yaliyopatikana kutokana na mauzo hayo.
Chama cha Imran Khan ambacho sasa kiko upande wa upinzani cha Pakistan Tehreek-e-Insaf kimelaani hukumu hiyo na kuitaja kuwa “ukurasa mbaya katika historia” na kuarifu kuwa Khan alikuwepo mahakamani wakati Jaji alipotangaza uamuzi huo katika gereza la Adiala mjini Rawalpindi anakozuiliwa.