Kampuni inayojishughulisha na huduma ya mikopo hapa nchini ya Platinum Credit Tanzania imeeleza kuwa tuzo iliyopata ya “Consumer Choice Awards Africa 2025”, imekuwa chachu kwao kuongeza ufanisi zaidi.
Kauli hiyo umetolewa na kuu wa kitengo cha biashara na mauzo kutoka katika Kampuni hiyo, Alan Luguza.
Akiwa Jijiji Dar es salaam, amesema ushindi walioupata umetoka kwa watanzania, na kuifanya taasisi hiyo kuwa taasisi bora ya kifedha kwa mwaka 2025.
”Tunawashukuru watanzania kwa kutupigia kura, lakini pia wateja wetu ambao ni wadau wetu wa kwanza, kutambua na kuthamini mchango wetu katika miaka yote ambayo tulikuwa katika oparesheni”.
Kwa upande wake Augustine Mpollo, ambaye ni Afisa bidhaa wa kampuni hiyo, amesema kutokana na huduma wanazozitoa wataendelea kuhakikisha wanaimarisha zaidi mazingira ya huduma ya mikopo hiyo.