Meli

Chanzo cha picha, X/Sec_Noem

Marekani imekamata meli ya mafuta ambayo ilikuwa imeondoka hivi karibuni kutoka Venezuela, kulingana na Wizara ya Usalama wa Ndani ya Marekani.

Ni mara ya pili mwezi huu Marekani kukamata meli ya kubeba mafuta nje ya pwani ya nchi hiyo.

Hatua hiyo inakuja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema Jumanne kwamba alikuwa akiamuru “kuzizuia” meli za mafuta zilizowekewa vikwazo zinazoingia na kutoka Venezuela.

Venezuela imelaani kukamatwa kwa meli zake hivi karibuni, ikielezea kuwa ni “wizi na utekaji nyara”. Venezuela hapo awali imeishutumu Marekani kwa kujaribu kuiba rasilimali zake.

“Vitendo hivi havitapita bure bila kuadhibiwa,” taarifa kutoka kwa serikali ya Venezuela ilisema, ikiongeza kuwa inakusudia kuwasilisha malalamiko kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na “mashirika mengine ya pande nyingi na serikali za dunia”.

Operesheni hiyo iliongozwa na Walinzi wa Pwani wa Marekani, sawa na operesheni iliyofanyika mapema mwezi huu.

Meli hiyo ilipandishwa na timu maalum ya kimkakati, na ilikuwa katika maji ya kimataifa ilipochukuliwa.

Unaweza kusoma;

  • Kwa nini Marekani inahusisha vita dhidi ya madawa ya kulevya na ugaidi?
  • Fahamu kuhusu meli ya mafuta iliyokamatwa na Marekani karibu na pwani ya Venezuela
  • Jinsi Venezuela inavyotumia ‘meli za mapepo’ kukwepa vikwazo vya mafuta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *