Jumuiya ya Maulamaa wa Yemeni ilifanya mkutano mkubwa katika mji mkuu Sanaa siku ya Jumamosi, na kusisitiza jukumu la kidini la wasomi na maulamaa katika kutetea Qur’an na matukufu ya Kiislamu.

Muungano huo umetoa wito wa kuhamasisha Umma wa  Kiislamu dhidi ya uchokozi wa Marekani na utawala wa Kizayuni, na kuchukua misimamo madhubuti dhidi ya kuidhalilisha Quran Tukufu.

Jumuiya ya Maulamaa wa Yemeni iilifanya mkutano mjini Sanaa chini ya kaulimbiu “Wajibu wa Wasomi katika Kutetea Kitabu cha Mungu na Matukufu na Kuhamasisha Umma kwa Jihad dhidi ya Marekani  na utawala vamizi wa Israel.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *