Michuano ya soka ya kombe la mataifa ya Afrika – AFCON 2025 inang’oa nanga nchini Morocco hivi leo Jumapili, kwa wenyeji Morocco kupambana na Comoros katika mchezo wa ufunguzi baadae usiku.

Morroco ina kibarua kigumu kwenye michuano hiyo kutokana na matumaini makubwa ya mashabiki wake ndani na nje huku nyota wake Achraf Hakimi akirejea kwenye dimba la michuano hiyo baada ya kuuguza kwa muda majeraha. Afrika Kusini kukutana na Misri, Nigeria kuvaana na Tunisia katika AFCON

Matarajio ya mashabiki yataipa Morocco kibarua kigumu
Matarajio ya mashabiki yataipa Morocco kibarua kigumuPicha: Gavin Barker/BackpagePix/empics/picture alliance

Miongoni mwa washindani wakubwa wa timu ya Morocco kwenye dimba hilo la michuano ya AFCON ni Senegal, Ivory Coast, Misri na Nigeria.

Ufunguzi kati ya Morocco dhidi ya Comoros utachezwa katika uwanja wa mwanamfalme Moulay Abdellah unaobeba watazamaji 69,000, mjini Rabat. Fainali ya michuano hiyo ya mwaka huu itachezwa Januari 18.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *