Marekani imesaini jana Jumamosi mpango wa kuimarisha mfumo wa afya nchini Nigeria, hatua ambayo inaashiria kurekebisha mahusiano yake na taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika.
Hii ni baada ya rais Donald Trump kuishambulia serikali ya Nigeria kwa madai kwamba inaruhusu mauaji ya wakristo. Mwenyekiti wa AU akanusha madai ya Trump kuhusu mauaji ya kimbari Nigeria
Chini ya mkataba huo wa miaka mitano kati ya mataifa hayo, Washington itachangia kiasi dola bilioni 2.1 kusimamia miradi ya kupambana na HIV, kifua kikuu, Malaria na Polio pamoja na kuendesha miradi ya afya ya uzazi na watoto.
Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Nigeria imeahidi kuongeza bajeti yake ya afya kufikia takriban dola bilioni 3 katika kipindi cha miaka mitano, huku Marekani ikisisitiza juu ya kushirikishwa zaidi Wakristo katika utoaji huduma hizo za afya.