Baraza la mawaziri wanaohusika na usalama nchini Israel limeidhinisha mpango wa ujenzi wa makaazi mapya 19 ya walowezi wa kiyahudi katika ardhi ya Wapalestina inayokaliwa kwa mabavu ya Ukingo wa Magharibi.

Hatua hii mpya inaifanya idadi jumla ya makaazi yaliyoidhinishwa kujengwa na Israel kwenye eneo hilo katika kipindi cha miaka mitatu kufikia 69, kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo Jumapili.Netanyahu

Sura ya makaazi makubwa zaidi ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi ya Maale Adumin
Sura ya makaazi makubwa zaidi ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi ya Maale Adumin Picha: Menahem Kahana/AFP/Getty Images

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri wa fedha Bezalel Smotrich imesema kwamba pendekezo lililoandaliwa na waziri huyo na mwenzake wa ulinzi Israel Katz la kutangaza rasmi ujenzi wa makaazi mapya 19 katika eneo la Judea na Samaria limeidhinishwa na baraza la mawaziri.Waziri wa Fedha wa Israel asema kuwa “Gaza itaangamizwa kabisa”

Kwa mujibu wa taarifa ya Smotrich, Israel itaendelea kujenga na kuchukuwa kile amekiita ardhi yao ya urithi kwa imani ya kufuata njia ya haki na kuzuia kujengwa kwa kile amekiita dola la magaidi la Palestina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *