Mkuu wa sera za nje wa rais wa Urusi Vladmir Putin, Yuri Ushakov amesema ana uhakika kwamba bado hakuna nafasi ya kupatikana amani katika mgogoro wa Ukraine kutokana na hatua iliyochukuliwa na Umoja wa Ulaya na Ukraine ya kufanya mabadiliko kwenye mapendekezo yaliyowasilishwa na Marekani.
Hayo yameripotiwa na shirika la habari la Interfax hivi leo, chini ya kiwingu cha mazungumzo yaliyofanyika jana Jumamosi kati ya wajumbe wa Marekani na Urusi huko Florida.
Mjumbe maalum wa rais Vladmir Putin kwenye mazungumzo hayo Kirill Dmitriev amewaambia waandishi habari baada ya mkutano na mjumbe maalum wa Marekani Steve Witkoff na mkwe wa rais Donald Trump, Jared Kushner kwamba mazungumzo hayo yamekwenda vizuri na yataendelea leo Jumapili. Duru nyingine ya mazungumzo ya amani kuhusu mzozo wa Ukraine yafanyika Miami
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema jana kwamba kwa sehemu kubwa maamuzi yao itategemea msimamo wa Marekani baada ya mazungumzo na Urusi.
Trump alianzisha juhudi pana za kidiplomasia kumaliza vita vya Ukraine lakini juhudi hizo zinakabiliwa na hali ngumu kutokana na madai yasiyolingana kati ya Moscow na Kiev.