Serikali ya Cambodia imearifu kwamba, zaidi ya watu nusu milioni nchini humo wameachwa bila makaazi kufuatia wiki mbili za machafuko yaliyosababisha umwagaji damu kati ya nchi hiyo na jirani yake Thailand. Asia 

Taarifa ya serikali ya mjini Phnom Penh imetolewa leo kuelekea mkutano wa kikanda ulioitishwa kwa lengo la kupunguza mvutano huo.

Wacambodia wakikimbilia kutafuta usalama wakiwa na misaada ya vyakula
Wacambodia wakikimbilia kutafuta usalama wakiwa na misaada ya vyakulaPicha: Sovannara/Xinhua News Agency/picture alliance

Mapigano mapya kati ya majirani hao wawili wa Kusini mashariki mwa Asia mwezi huu yaliyohusisha vifaru vya kijeshi, droni na makombora yamesababisha watu 22 kuuwawa upande wa Thailand na 19 nchini Cambodia.Thailand yaweka marufuku ya kutokutoka nje wakati mapigano na Cambodia yakiendelea

Chanzo cha machafuko hayo ni eneo la mpakani la kilomita 800 linalojumuisha gofu la hekalu la kale lililoachwa na wakoloni.

Cambodia na Thailand zimesema mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa kanda hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia utakaongozwa na Malaysia kesho unatarajiwa kuutatuwa mvutano huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *