Kitengo cha Huduma za Ajira cha Ofisi ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano kimetakiwa kuwaunganisha vijana na fursa za ajira ndani na nje ya nchi ili kupunguza wigo wa vijana wenye taaluma na ujuzi ambao hawana ajira nchini.

Akitoa maagizo hayo kwa watendaji wa kitengo hicho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu amesema kuwa ni wajibu wa kitengo hicho kuwasaidia watafuta ajira na waajiri na kuwaunganisha kwa ajili ya mafanikio ya pande zote.

“Serikali inapokea wawekezaji ambao huja na forsa nyingi za ajira zikiwemo za ndani na nje ya nchi huku kitengo hiki ikiwa na uwezo wa kufahamu vigezo na mahitaji ya ajira na kina uwezo wa kuwaunganisha vijana wanaokidhi vigezo na ajira na fursa hizo na hilo litapunguza idadi ya watu wasio na kazi hususani vijana” amesema Sangu

Vilevile Sangu ametaka kitengo hicho kuhakikisha kinawafahamisha wananchi hususani vijana kwa wakati kuhusu fursa za ajira ambazo serikali imezitafuta ndani na nje ya nchi.

Mbali na hayo kitengo hicho kimeshauriwa kuanzisha ‘application’ ili kurahisisha utoaji wa taarifa kwa vijana ambayo itawezesha vijana kuchangamkia fursa za ajira kwa urahisi.

Imeandaliwa na @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *