Wananchi wa Kijiji cha Sitalike, kilichopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi, wameiomba Serikali kushirikiana nao katika ujenzi wa masoko maalumu yatakayowawezesha kuuza bidhaa mbalimbali za asili kwa watalii, hususan wa kimataifa.
Wananchi hao wamesema kuwa kukosekana kwa masoko ya uhakika kunawanyima fursa muhimu za kibiashara, hali inayochangia kudorora kwa shughuli zao za kiuchumi na uwezo wao wa kujikimu kimaisha, licha ya kijiji chao kuwa katika eneo lenye mvuto mkubwa wa utalii.
Kauli hiyo imetolewa na wananchi hao wakati wakizungumza na waandishi wa habari, ikiwa ni sehemu ya shughuli za Kampeni ya Shangwe la Sikukuu, iliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na wadau wa utalii, ambapo wananchi wa ndani walipata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
✍ Mwanaidi Waziri
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates