Katika kaya nyingi za Mkoa wa Tanga, vihangaisho vilikuwa zaidi ya mapambo ya ndani; vilibeba ujumbe, historia na maadili ya jamii. Kupitia michoro na alama zake, wahenga waliwasilisha maonyo, mafundisho ya maisha na utambulisho wa jamii, bila kuhitaji maneno mengi.

Lakini kadri utandawazi unavyoendelea kushika kasi, utamaduni huo umeanza kufifia. Vihangaisho vinazidi kubadilishwa na mapambo ya kisasa, huku maarifa ya maana na ujumbe uliokuwa ukifichwa ndani ya sanaa hiyo yakipotea taratibu.

Wazee wa zamani wa Mkoa wa Tanga wanasema kizazi cha sasa hakitambui tena thamani ya vihangaisho kama lugha ya utamaduni na daraja la kuunganisha jamii.

Mariam Shedafa ana simulizi zaidi.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *