“AFCON kufanyika kila baada ya miaka minne ni nafasi kwa Afrika kuendelea kukua. Kila mashindano yatakuwa yakiboresha mpira wa Afrika, kwenye maeneo kama uwezo, uendeshaji bora pamoja na muonekano (wa mashindano yenyewe).” – Kocha wa Morocco Walid Regragui akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu maoni yake juu ya mabadiliko ya michuano ya AFCON baada ya 2028 ambapo itakuwa ikifanyika kila baada ya miaka minne.
Regragui amezungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Comoro ambapo wameshinda kwa mabao 2-0.
#AFCON2025 #AFCON25