Chanzo cha picha, Getty Images
Muda wa kusoma: Dakika 2
Iwapo jeraha la mshambuliaji wa Sweden, Alexander Isak (26), litathibitika kuwa kubwa kama inavyohofiwa, Liverpool huenda wakabadili mwelekeo na kutumia fedha zilizotengwa kumsajili mchezaji mwingine, winga wa Bournemouth na Ghana, Antoine Semenyo (25). (Telegraph)
West Ham wameonesha nia ya kumnunua mwezi Januari mshambuliaji wa Wolves na Norway, Jorgen Strand Larsen, mwenye umri wa miaka 25. (Athletic)
Aston Villa wamejiunga na klabu nyingine kwenye mbio za kumsajili beki wa Wolves na Norway, David Moller Wolfe, mwenye umri wa miaka 23, katika dirisha la usajili la Januari. (Football Insider)
West Ham na AC Milan wako kwenye mazungumzo ya kina kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Ujerumani, Niclas Füllkrug (32). (Sky Sports)
Chelsea wanatafuta kuwashinda wapinzani wao wa Ulaya katika mbio za kumsajili kiungo wa Genk na Ugiriki mwenye umri wa miaka 18, Konstantinos Karetsas. (Teamtalk)
Liverpool na Manchester United ni miongoni mwa klabu kubwa zinazomfuatilia kiungo wa Lille na Ufaransa mwenye umri wa miaka 18, Ayyoub Bouaddi. (CaughtOffside)
Wakati huo huo, beki wa kati wa Ufaransa Axel Disasi (27) ataondoka Chelsea Januari, huku klabu kadhaa tayari zikifuatilia upatikanaji wake. (Fabrizio Romano)
Tottenham hawajapokea ofa yoyote kutoka Fiorentina, licha ya ripoti kadhaa kutoka Italia kudai kuwa Fabio Paratici yuko tayari kukubali mkataba wa miaka mitano kuwa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ya Serie A. (Mail)