
Uwasilishaji faili jipya la mahakama katika kesi ya Jeffrey Epstein unaonyesha kwamba, mfanyabiashara haramu huyo wa ngono alimtambulisha binti wa miaka 14 kwa Rais wa Marekani Donald Trump katika makazi yake ya Mar-a-Lago.
Hati hiyo ya mahakama iliyotolewa Ijumaa inahusiana na tukio la 1990 wakati Epstein alimpiga kiwiko Trump wakati akimuarifisha kwa msichana wa miaka 14, ambaye alitambuliwa kama ‘Jane Doe.’
Wakati wa uarifishaji huo, Epstein “alimwuliza Trump kwa mzaha,” akimkusudia msichana huyo, “Huyu ni mzuri, sivyo?” hati hiyo ya mahakama imefichua. Kwa mujibu wa nyaraka hizo za mahakama, Trump alitabasamu na kuashiria kuafikiana na Epstein kwa kutikisa kichwa.
Katika malalamiko yake ya 2020 kwa mahakama, mwathirika anasema alinyanyaswa kwa miaka kadhaa na Epstein. Hata hivyo, Trump hakutajwa kuwa alimdhulumu mwanamke huyo akiwa binti, katika nyaraka 300,000 zinazohusiana na faili la Epstein ambazo ziliwekwa paruwanja Ijumaa.
Wanachama wa chama cha Democratic katika Congress ya Marekani walifichua hivi karibuni picha zinazomdhihirisha Trump, Rais wa zamani Bill Clinton, mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates na watu wengine wenye ushawishi wakiwa pamoja na mfanyabiashara aliyepatikana na hatia ya kufanya biashara haramu ya ngono ya watoto, Jeffrey Epstein.
Epstein anadaiwa kujiua gerezani mnamo 2019 akisubiri kusikilizwa kesi yake ya mashtaka ya biashara ya ngono. Hata hivyo mawakili wa Epstein wanapinga matokeo ya uchunguzi wa sababu ya kifo chake wakisema kuwa kuna shaka kubwa kuhusu chanzo halisi cha kifo hicho, na hivyo kuchochea dhana kuwa aliuawa.
Ni vyema kuashiria hapa kuwa, nyaraka zinazohusiana na Jeffrey Epstein, bepari na bilionea aliyepatikana na hatia ya biashara ya ngono ya watoto, zimeanika peupe uhusiano wa siri aliokuwa nao na watu mashuhuri na vilevile shirika la ujasusi la utawala haramu wa Israel, Mossad.