Michuano ya kandanda kwa mataifa ya Afrika, AFCON 2025, imeanza usiku wa kuamkia leo na katika mechi ya ufunguzi wenyeji Morocco waiiburuza timu ya taifa ya visiwa vya Commoro mabao 2-0.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum huko Rabat,

Katika uwanja soka wa Prince Moulay Abdellah uliojaa watu na wenye shauku, Morocco ilicheza kwa kipindi ha kwanza katika mechi yake ya ufunguzi ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 dhidi ya Comoro. Lakini baada ya mapumziko, Atlas Lions walipata waliweza kufaulu kxa kupata ushindi wa 2-0 huko Rabat,  bao lililoofungwa na Brahim Diaz na bao la pili la kushangaza kutoka kwa Ayoub El Kaabi.

Kazi imekamilika kwa Morocco. Wakizingatiwa miongoni mwa wanaopigiwa upatu kwa AFCON hii ya 2025, vjana wa Walid Regragui walitaka kushinda mechi yao ya ufunguzi na kuthibitisha kwamba wanaweza kukabiliana na shinikizo. Tutaangalia kwa karibu sehemu iliyobaki ya mashindano ili kuona kama wanaweza kufanya vizuri. Lakini lengo kuu limetimizwa: Morocco inaondoka na pointi tatu na kuwa na imani zaidi baada ya mechi hii ya kwanza.

Rahimi akosa penalti mapema

Bila Achraf Hakimi, aliyekuwepo kupokea kombe lake la Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka 2025 lakini aliyeachwa benchi na kocha wake, timu ya taifa ya Morocco ilianza mashindano yake ya AFCON katika mazingira ya kipekee. Katika uwanja mpya na mzuri, makumi ya maelfu ya mashabiki wenye shauku walikuwepo kuwashangilia. Hata hivyo, mvua kubwa kwa ilikuwa ikinyesha.

Wakitawala tangu mwanzo, Morocco walikatishwa tamaa walipokosa fursa yao ya kwanza ya kufungua bao. Soufiane Rahimi, kutokana na penalti iliyotolewa baada ya faulo ya mchezaji wa Comoro Iyad Mohamed kwa Brahim Diaz, aliona shuti lake moja kwa moja katikati likiokolewa na goti la kipa Yannick Pandor (dakika ya 11). Kisha, Romain Saïss, alilazimika kuondoka uwanjani baada ya dakika kumi na tano tu kutokana na jeraha.

Kwa kuwa hawakufanikiwa sana katika kipindi cha kwanza (shuti moja tu lililolenga lango… na penalti iliyokosa), Wamorocco waliingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakati wa mapumziko huku wakiendelea kupewa moyo na mashabiki wake. Kizuizi cha ulinzi kutoka timu ya Comoro kilisimama imara (20% kutawala mpira), na Coelacanths wangeweza hata kufungua bao katika dakika za mwisho kama isingekuwa Yassine Bounou kuokoa lango lake.

Diaz apachika bao la kwanza

Baada ya mapumziko, Atlas Lions walitawala mpira na hatimaye wakatoboa ulinzi wa Comoro. Noussaïr Mazraoui, akiwa amekwama upande wa kulia wa eneo la hatari, alimtengenezea Brahim Diaz, na kiungo mshambuliaji wa Real Madrid akatoa shuti lililowekwa vizuri na kuipeleka Morocco kwenye furaha (dakika ya 55). 

Baada ya kuingia dakika kumi mapema kuchukua nafasi ya Rahimi, Ayoub El Kaabi alifunga bao la pili kwa sarakasi nzuri baada ya krosi kutoka kwa Anass Salah-Eddine (dakika ya 74). Inatosha kuthibitisha ushindi, ingawa Comoro wenye ujasiri walijaribu kusimama imara hadi dakika ya mwisho.

Kwa ushindi huu uliostahili hatimaye, Morocco sasa inaweza kutarajia ushindi mwingine kwa mechi yao ijayo dhidi ya Mali mnamo Desemba 26. Wakati huo huo, Comoro italazimika kumenyana na Zambia siku hiyo huko Casablanca.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *