Saar ametoa matamshi hayo wiki moja baada ya Wayahudi 15 kupigwa risasi na kuuawa kwenye mkusanyiko wa kuadhimisha tukio la kidini mjini Sydney, Australia.

Akizungumza kwenye tukio la kuwasha mishumaa kukamilisha tamasha la Kiyahudi liitwalo Hanukkah, Saar amesema, ingawa Wayahudi wanayo haki ya kuishi kwa usalama kote duniani, hivi sasa lakini jamii hiyo ikiwemo kwenye mataifa ya Uingereza, Ufaransa, Australia, Canada na Ubelgiji “imekuwa ikiwindwa”.

Tangu kuzuka vita vya Gaza vilivyofuatia shambulizi la kundi la Hamas la Oktoba 07, 2023, viongozi wa Israel wameonya mara kadhaa kuwa chuki dhidi ya Wayahudi inaongezeka kwenye nchi za magharibi na kuzituhumu serikali za mataifa hayo kushindwa kudhibiti hali hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *