Msemaji wa Ikulu ya Nigeria ametoa taarifa hizo kupitia ujumbe kwenye mtandao wa X, bila hata hivyo kufafanua namna serikali ilivyofanikisha kuachiwa wanafunzi hao.

Afisa huyo amesema, kuachiwa kwao kunahitimisha zoezi la kuwarejesha nyumbani wanafunzi wote waliotekwa nyara kwenye shule ya St. Mary´s iliyopo katika jimbo kaskazini la Niger. 

Ilikadiriwa zaidi ya wanafunzi 300 walichukuliwa mateka na wapatao 100 tayari waliachiwa huru mapema mwezi huu.

Miaka ya hivi karibuni, Nigeria imekuwa ikipambana na matukio mengi ya utekaji nyara yanayofanywa na wanamgambo wa itikadi kali au magenge ya majambazi kwa lengo la kujipatia fedha ya kikomboleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *